Simba yateuliwa na CAF kuwania tuzo ya klabu bora Afrika 2025.
Joyce Shedrack
October 22, 2025
Share :
Klabu ya Simba imeingia rasmi kwenye orodha ya vilabu 10 bora barani Afrika vinavyowania tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka ya Wanaume 2025 zinazotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika CAF.

Simba ambao msimu uliopita walifika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wanawania tuzo hiyo na vilabu vingine tisa ambavyo ni
CR Belouizdad
CS Constantine
ASEC Mimosas
Pyramids
RS Berkane
Mamelodi Sundowns
Orlando Pirates
Stellenbosch
Al Hilal
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka huu katika hafla maalum ya CAF Awards 2025.





