pmbet

Simba yateuliwa rasmi kuwa Balozi wa Utalii Zanzibar

Eric Buyanza

January 5, 2024
Share :

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Mohammed Said ameiteua Simba Sports Club kuwa Balozi wa Utalii wa Zanzibar.
 

Waziri Simai amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango mkubwa klabu ya Simba inatoa katika kutangaza utalii wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
 

Klabu ya Simba ilianzisha mkakati wa kuitangaza Zanzibar kupitia kauli mbiu ya Visit Zanzibar katika jezi na mitandao yake ya kijamii wakati huu wa Kombe la Mapinduzi.
 

Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Simba Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula alisema,“ tunaishukuru sana Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar kwa kutambua mchango wa timu yetu kutangaza utalii hivyo kukuza uchumi wa Zanzibar, tunaona fahari kubwa kuwa sehemu ya maendeleo makubwa Zanzibar inayoyapata.”
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet