pmbet

Simbu abeba medali ya nafasi ya pili Boston Marathon

Sisti Herman

April 22, 2025
Share :

 

Mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu ameandika historia mpya katika mbio za kilomita 42 kwa kushika nafasi ya pili mbio za Boston Marathon zilizofanyika leo, Aprili 21, 2025, huko Massachusetts, Marekani.

Simbu, ambaye amekuwa akiiwakilisha Tanzania kwa mafanikio katika medani za kimataifa, alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2:05:04, akitanguliwa kwa sekunde chache na Mkenya John Korir aliyeibuka kidedea kwa muda wa saa 2:04:45 ikiwa ni muda wa pili kwa kasi zaidi katika historia ya mbio hizo.

Katika mbio hizo, Simbu alionesha ushupavu wa hali ya juu, akiibuka kinara kutoka kwa kundi kubwa la wanariadha waliotabiriwa kufanya vizuri, akiwemo Cybrian Kotut wa Kenya aliyeshika nafasi ya tatu na Mmarekani Conner Mantz aliyemaliza wa nne.

Akizungumza baada ya mbio hizo, Simbu amesema kuwa alikuwa amejiandaa vizuri na anaamini bado ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi katika mbio zijazo.

“Nashukuru Mungu kwa kunipa nguvu. Hii ni zawadi kwa Watanzania wote. Nilipambana hadi mwisho, na nafasi ya pili ni fahari kubwa kwangu na kwa taifa,” amesema Simbu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet