Simbu ashika nafasi ya 3 Marathon Korea
Sisti Herman
April 7, 2024
Share :
Mwanariadha wa Tanzania Alphonse Simbu ameshika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Daegu Marathon 2024 nchini Korea kusini yaliyomalizika hivi punde huku akizidiwa na wanariadha wawili raia wa Kenya, Stephane Kiprop na Kennedy Kimutai walioshika nafasi ya kwanza na ya pili.
Simbu anayejiandaa na michuano ya Olympic mwaka huu yatakayofanyika na Paris nchini Ufaransa kwenye mbio hizo za leo alikimbia umbali wa kilomita 42 kwa saa 2:07:55, akizidiwa sekunde 50 tu na mshindi wa kwanza.