pmbet

Simbu atwaa medali ya shaba Burj 2 Burj half Marathon

Sisti Herman

February 8, 2026
Share :

 

Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Alphonce Simbu ameendelea kufanya vizuri kimataifa baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya mbio fupi (Burj 2 Burj half Marathon) yaliyofanyika alfajiri ya leo nchini Dubai, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Joshua Cheptegei (Uganda).

Mwanariadha huyo alikimbia umbali wa kilometa 21 na dakika 59 na sekunde 30, huku akimuacha mbali mpinzani wake, Enos Kipruto kutoka nchini Kenya aliyeshika nafasi ya nne.

Mashindano hayo yalishirikisha wanariadha kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia pamoja na Ujerumani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet