Simon Msuva anga’ra Saudia
Joyce Shedrack
March 6, 2024
Share :
Mchezaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya AL Najma ya ligi daraja la pili nchini Saudia Arabia Simon Happygod Msuva (30) amefunga magoli mawili katika mchezo ulioikutanisha timu yake na klabu ya AL Arab na kukubali kipigo cha magoli 5 kwa 2.
Msuva alifunga magoli pekee ya timu yake katika mchezo huo dakika ya 52 na 65 wakati timu yake ikiwa nyuma kwa magoli 3 kwa 0 kabla ya kuja kuongezewa mengine mawili na kufanya mchezo huo kutamatika kwa goli 5-2.
Hadi hivi sasa tangu asajiliwe na klabu hiyo Msuva amecheza mechi 2 na kufunga magoli 3.
Klabu ya Al Najma inashika nafasi ya 9, ikiwa imekusanya alama 23 katika michezo 24 iliyocheza ya ligi daraja la pili nchini Saudia Arabia.