Simu ya Raila Odinga yazua gumzo mitandaoni!
Eric Buyanza
January 16, 2024
Share :
Video iliyosambaa kutoka Tiktok ikionyesha simu ya mwanasiasa nguli wa Kenya, Raila Odinga ikiwa imefungwa rubber band imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii Afrika mashariki.
Kwenye video hiyo mwanasiasa huyo mkongwe aliyeukosa kiduchu tu Urais wa Kenya, anaonekana akiongea jambo mbele za watu huku akiwa na furaha na mbele yake akiwa ameweka simu yake iliyofungwa na mpira (Rubber band).
Wananchi wengi waliotoa maoni yao mitandaoni wameonekana kushangazwa na mtu mkubwa kama Raila kutumia simu ya hivyo ili hali ana uwezo wa kuwa na simu ya aina yoyote anayotaka.