Simu ziite...! Yanga vs Mamelodi ni MUDA DAY
Sisti Herman
March 25, 2024
Share :
Klabu ya Yanga kupitia afisa habari na mawasiliano wao imethibitisha kuwa wameupa mchezo wao wa robo fainali ya mabingwa Afrika dhidi ya Mamelod Sundowns jina la "Muda Day" kama sehemu ya hamasa na kumpa heshima kiungo wao wa kati Mudathir Yahya ambaye amekuwa na mchango mkubwa mabao kwa siku za karibuni.
Hadi sasa Mudathir kwenye ligi ya mabingwa kati ya michezo minne aliyocheza msimu huu amefunga magoli mawili akiingia kwenye kikosi cha wiki mara moja.
Staili yake maarufu ya kushangilia ni kupiga simu huku akitumia kilinda ugoko kama mfano wa simu.