pmbet

SIMULIZI YA LORNA: Mkenya anayebebea watu wengine ujauzito

Eric Buyanza

September 8, 2026
Share :

Katika jamii nyingi za Kiafrika, suala la mwanamke kubeba ujauzito kwa niaba ya mtu mwingine (surrogacy) bado ni geni na limegubikwa na usiri mkubwa. Hata hivyo, mwanamke mmoja nchini Kenya aitwaye Lorna Fidelia, aliamua kuvunja ukimya huo na kushirikisha ulimwengu safari yake ya kipekee kama mama mbeba ujauzito wa kukodi.

 

Uamuzi Lorna kuingia kwenye kazi ya kubeba ujauzito wa wengine ulisukumwa na mambo makuu mawili:

 

1. Kusaidia familia zinazohangaika na changamoto ya ugumba kupata watoto.

2. Kupata msaada wa kifedha utakaomsaidia kukidhi mahitaji ya kimsingi na kusomesha watoto wake.
 

Mchakato wa Lorna ulianza katika kliniki ya Nairobi IVF. Kwa mujibu wa mkataba wao wa awali na wazazi walengwa, makubaliano yalikuwa ni Lorna kubeba mtoto mmoja tu. Hata hivyo, viinitete (embryos) vilivyopandikizwa mwilini mwake vilishika kwa mafanikio makubwa na kujigawa, jambo lililopelekea kupata ujauzito wa watoto watatu (mapacha watatu). Licha ya mshtuko na ugumu wa kubeba mimba ya aina hiyo, Lorna alihimili changamoto zote za kiafya hadi siku ya kujifungua.
 

Safari ya Lornahata hivyo iliibua mijadala mikubwa kuhusu muongozo za surrogacy nchini Kenya kwani mkataba wao wa awali haukujumuisha kipengele cha Lorna kunyonyesha watoto baada ya kuzaliwa. Lakini kwa sababu watoto walizaliwa kabla ya muda wao (njiti - wiki 34) na kuwekwa ICU, madaktari walishauri wapewe maziwa ya mama. Ilibidi mkataba ufanyiwe marekebisho ya haraka ili kuruhusu Lorna kutoa maziwa yake kwa ajili ya watoto hao kwa miezi kadhaa.

 

Baada ya kuwakabidhi watoto hao watatu salama kwa wazazi wao, Lorna ameweka wazi kuwa uzoefu huo haukumkatisha tamaa. Badala yake, yuko tayari na ana nia ya kufanya mchakato huo tena kwa ajili ya familia nyingine inayohitaji msaada, akiamini kuwa hii ni huduma muhimu na kazi halali inayobadili maisha ya watu.

 

Kisa cha Lorna kimekuwa chachu ya mabadiliko, kikiwemo kichocheo cha miswada mbalimbali ya sheria bungeni nchini Kenya inayolenga kulinda haki za akina mama wabeba ujauzito, wazazi walengwa, na watoto wanaozaliwa kupitia njia hii.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet