Sina damu mikononi mwangu - Ruto
Eric Buyanza
July 1, 2024
Share :
Rais wa Kenya William Ruto amesema hana damu mikononi mwake kufuatia mauaji ya watu yaliyoshuhudiwa wakati wa maandamano yaliyofanyika hivi karibuni kupinga ongezeko jipya la kodi iliyopendekezwa katika Mswada wa Fedha wa 2024.
Akizungumza na wanahabari Ikulu ya Kenya jana Jumapili, Juni 30, Ruto amesema polisi walitekeleza majukumu yao kwa uhuru wao wakati wa maandamano hayo.
“Maisha yoyote ya Mkenya yaliyopotea yananisumbua, na ndiyo sababu nilipochaguliwa nilisema kwamba hakutakuwa na mauaji ya kiholela nchini Kenya. Pia nilihakikisha kuna Huduma Huru ya Polisi na kutia sahihi vyombo vinavyofaa kwa polisi kufanya kazi kwa uhuru,” alisema Ruto.