pmbet

Sina 'Pengo', ule ni ubunifu tu – Joti

Eric Buyanza

April 2, 2025
Share :

Mchekeshaji maarufu nchini, Lucas Mhavile 'Joti' amekuwa akibuni staili mbalimbali za kuigiza ambazo zinawavutia wengi, mojawapo ni ule muonekano wa pengo ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza Je! ni pengo kweli au kuna jambo amefanya?

 

Haya hapa majibu ya Joti;

 

“Huwa nakutana sana maswali ya watu tofauti kuhusu meno yangu kama nina pengo lililooza au jeusi. Watu wanafikra tofauti na kuniona nina pengo jeusi, ila mimi meno yangu yote ni meupe peee... lile pengo jeusi linaloonekana huwa nafanya ubunifu kwa ajili ya sanaa yangu na nashukuru hii staili imewateka watu wengi sana kudhani nina pengo jeusi au lililooza."

 

"Unajua kwenye sanaa, lazima uwe na ubunifu, ndiyo maana katika kujitafuta nimepitia mbinu nyingi sana ilimradi tu niweze kuwateka mashabiki zangu, hivyo mimi sina pengo bana, leo acha niwaambie tu ukweli," alisema Joti.

 

MWANASPOTI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet