pmbet

Sina Pressure - Hemed Morocco

Sisti Herman

January 21, 2024
Share :

Kaimu kocha mkuu wa kikosi cha Taifa Stars Hemed Suleiman ameweka wazi kuwa kuelekea katika mchezo ujao wa fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Zambia anaamini wataenda kufanya vizuri.

 

Hemedi na msaidizi wake Mgunda imani yao ni kuwa wachezaji walionao kambini ni wazuri na wanaweza kuwapa matokeo mazuri kilichobaki wanahitaji kusukumwa tu kidogo.

 

“Kwangu mimi haina presha kwasababu nishakuwa kocha mkuu kwa timu tofauti”.

 

“Nishakuwa timu ya Taifa kwa takribani miaka 10 sasa, mashindano yote ambayo imeshiriki mimi nineshiriki pia, kwahiyo hakuna presha kabisa kwangu mimi”.

 

“Nitajaribu kutoa kile ambacho tunacho na kile ambacho tumekipata kwenye mashindano haya na naamini tuna wachezaji wazuri wanataka kusukumwa tu kidogo, nafikiri tutafanya vizuri mechi inayofuata”, Alisema Hemed Suleiman.

 

Tanzania ina kibarua cha pili kesho dhidi ya Zambia kwenye kundi F la michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea huko nchini Ivory Coast.

Hadi hivi sasa Taifa Stars haina alama yoyote baada ya kupoteza mchezo wa kwanza 3-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco.

 

Tanzania imebakiwa na michezo miwili dhidi ya Zambia ambao utachezwa kesho jumapili na dhidi ya DR Congo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet