Sina uadui na P-Funk - Master Jay
Sisti Herman
December 15, 2023
Share :
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Master J kwenye mahojiano maalum na PMTV amebainisha wazi kuwa hana uadui na mtayarishaji mwenzake nguli P-Funk Majani kama watu wengi wanavyodhani.
"Watu wengi wanajua mimi na P-Funk ni maadui, hapa sisi ni marafiki, tumetoka mbali sana, tulikua tukiamka asubuhi tunajuliana hali, yeye alikua mpambe kwenye harusi yangu, tuna historia nzuri" alisema Master J.
Fuatilia kwa undani mahojiano haya kupitia mtandao wa Youtube wa PMTV.