Singeli ni Nembo ya Tanzania, Hatumuachii mtu! - Gerson Msigwa
Joyce Shedrack
March 11, 2024
Share :
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo Gerson Msigwa ametoa onyo kwa watu wa Mataifa mengine wanaosema muziki wa singeli ni wa kwao na kusema muziki huo ni nembo ya Taifa la Tanzania na wataendelea kuulinda.
Msigwa amesema mziki wa singeli ni wa watanzania na amewapongeza wasanii wote wa singeli kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya huku akiwaahidi kuwalinda.
“Singeli ni mziki wetu Tanzania na tunataka kuandaa siku yake, tunao wadau wanataka kuandaa tamasha tutaangalia namna bora ya kufanya hii singeli hatumuachii mtu asije akajitokeza mtu akasema ni ya kwao haiwezekani”. Amesema Msigwa
Akizungumzia mchakato wa kupatikana kwa mdundo wa Taifa Msigwa amesema mchakato huo bado unaendelea lakini kuna vivunge (kits) zaidi ya 400 vipo BASATA na amewataka wasanii watumie (kits) vivunge hivyo kwenye nyimbo zao ili kuweka vionjo vya tofauti na kuutambulisha muziki wa Tanzania .