pmbet

Singida Black Stars yaipa onyo Yanga.

Joyce Shedrack

October 28, 2024
Share :

Nawakumbusha wapinzani wetu Young Africans wasijiamini kupitiliza wakaona mechi hii ni mechi ya kawaida. Hatuongozi ligi kwa bahati mbaya. Nimesikia maneno ya Ali Kamwe mara kwa mara anazungumza kama anakuja kucheza na timu ya mtaani tu. Achunge sana kauli zake.

Pia mashabiki wasije na matokeo yao mfukoni. Huu ni mpira wa miguu. Kama kuna mtu anaenda kuweka bondi nyumba, mke au biashara yake kwamba Singida Black Stars lazima tufungwe basi awe tayari kwa lolote.

Tunafahamu tunaenda kucheza mechi ngumu na tutawaheshimu Yanga lakini tunao uwezo wa kupambana hadi tone la mwisho.

Viingilio vya mechi tumeshatangaza ni shilingi 5000 (Jukwaa la Saa/Orbit) 10,000 (Jukwaa la Urusi) 15,000 (Wings) na 20,000 (VIP).

Hii ni mechi inayokutanisha timu mbili ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja kwahiyo watu wasitegemee itakuwa mechi rahisi au mechi ya upande mmoja. Msimu huu tumeshasema INAWEZEKANA na tunamaanisha.

Ameyasema hayo Afisa Habari wa Singida Black Stars Hussein Massanza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet