Singida Black Stars yanasa saini ya Serge Pokou kutoka Al Hilal.
Joyce Shedrack
January 16, 2025
Share :
Klabu ya Singida Black Stars imemtambulisha kiungo mshambuliaji raia wa Ivory Coast Serge Pokou kutoka Al Hilal kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na winga wa kushoto pamoja na nafasi ya shambuliaji wa kati.
Pokou aliwahi kuitumikia Asec Mimosas kabla ya kujiunga na Al Hilal Julai 2024.