Singida BS yathibitisha kumtoa kwa mkopo Mossi Nduwumwe.
Joyce Shedrack
August 7, 2026
Share :
Klabu ya Singida BS kupitia msemaji wake Hussein Massanza imethibitisha kumtoa kwa mkopo wa msimu mmoja mchezaji wao Mossi Nduwumwe kwenda klabu ya MC Alger ya Algeria.

“Ni kweli tumemtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja mchezaji wetu @nduwumwe_mossi kwenda MC Alger ya Algeria kwa msimu wa 2026/27”.
“Huu sio mkopo wa bure, bali ni mkopo wenye ada ya uhamisho (paid loan) unaozinufaisha pande zote”.
1. Klabu itanufaika kwa mapato ya ada ya mkopo
2. Mchezaji anapata fursa ya kuongeza experience na kuimarisha kiwango chake katika mazingira ya ushindani mkubwa zaidi.
“Tunamtakia mchezaji wetu kila la kheri na tunaamini ataiwakilisha vyema Singida BS” Ameandika Hussein Massanza.





