pmbet

Singida na Coastal kufungua pazia la Kagame Cup leo

Sisti Herman

July 9, 2024
Share :

Timu mbili zinazowakilisha Ligi kuu Tanzania bara kwenye michuano ya Kombe la klabu Bingwa Afrika mashariki na kati (CECAFA Kagame Cup) Singida Black Stars na Coastal Union leo watacheza rasmi mechi zao za kwanza za hatua ya makundi.

Coastal Union ambao wapo kundi A wacheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya klabu ya Dekahadaha Fc kwenye dimba la KMC Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.

Singida Black Stars ambao wapo kundi C watacheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya APR kwenye dimba la Azam Complex kuanzia saa 3 kamili usiku.

Coastal Union ambao walimaliza nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ambao pia ni wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la shirikisho Afrika wapo kundi A wakiwa na timu za Al Wahdi ya Sudan, JKU ya Zanzibar na Dekedaha ya Somalia.

Singida Black Stars ambao walimaliza nafasi ya 7 kwenye ligi kuu Tanzania bara wakifahamika kama Ihefu wapo kundi C wakiwa na timu za El Merrikh ya Sudan, APR ya Rwanda na SC Villa ya Uganda.

Kundi lingine kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 9 ni kundi B ambalo lina timu za Al Hilal ya Sudan, Gor Mahia ya Kenya, Red Arrows ya Zambia na Telecom ya Djibout.

Michuano hiyo itachezwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi na KMC Mwenge.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet