Singida wakunja Mil 73 za taji la CECAFA Kagame Cup
Sisti Herman
September 15, 2025
Share :
Vigogo wa Sudan, Al Hilal SC wanatarajiwa kumenyana na Singida Black Stars ya Tanzania katika mchezo wa fainali ya michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025 leo Septemba 15, kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Katika nusu-fainali Jumamosi, Septemba 13, Al Hilal SC ililipiza kisasi cha kushindwa kwao katika nusu-fainali ya 2024 dhidi ya APR FC ya Rwanda kwa kuichapa 3-1.
Timu ya Singida Black Stars imefanikiwa kutinga fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo mwingine wa nusu fainali.
Zawadi za washindi kwa udhamini wa Rais wa Rwanda Paul Kagame:
Kiasi cha Tuzo (USD)
Mshindi $30,000 (zaidi ya Tsh 73 Mil.)
Mshindi wa pili $20,000 (zaidi ya Tsh 49 Mil.)
Nafasi ya tatu $10,000 (zaidi ya Tsh 24 Mil.)
Kombe rasmi la michuano hiyo lipo kwenye picha juu.