pmbet

Singida wawaalika Aigle Noirs Singida Big Day

Sisti Herman

July 25, 2024
Share :

Klabu ya Sindiga Black starskuelekea kilele cha siku ya “BIG DAY” ambayo hutumika kuwatambulisha nyota wapya kwaajili ya msimu wa 2024-25 wa ligi imewaalika klabu ya Aigle Noir ya Burundi kucheza mchezo wa kirafiki utachezwa Agosti 10,2024.

Aigle Noir ambayo ilimaliza nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu Burundi, itacheza mtanange huo ikiwa ni pamoja na kuwapima wachezaji wake kuelekea msimu mpya 2024/2025.

Ikiwa chini ya kocha Jimmy Ndayizeye, inatarajia kusafiri leo Julai 24,2024 kuelekea nchini Tanzania kuweka kambi ya siku kumi na nane.

Tai hao weusi wamecheza mchezo mmoja na kupoteza baada ya kuchapwa na Musongati FC mabao 2-0 kwenye uwanja wa NPPC mkoani Makamba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet