pmbet

Singida yafungiwa FIFA

Eric Buyanza

December 11, 2023
Share :

Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limeifungia Klabu ya Ligi Kuu ya Singida Fountain Gate FC kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Rodrigo Figueiredo Carvalho.
 

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imeendelea kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Carvalho kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
 

Nyota huyo raia wa Brazil alifunqua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara ambapo Singida ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.
 

“Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.” imesema taarifa ya TFF.
 

Singida Fontaine Gate FC inakumbwa na rungu la FIFA kwa mara ya pili chini ya siku nne zilizopita.
 

Itakumbukwa FIFA iliiifungia Wakulima hao wa Alizeti kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Pascal Serge Wawa mnamo Desemba 7, 2023 baada ya nyota huyo raia wa Ivory Coast kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
 

TEF inazitaka klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet