Sinza ya 2046 ni ya mwaka wa mbele
Sisti Herman
February 10, 2026
Share :

Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imekuja na mpango wa uendelezaji Upya wa eneo la Sinza kwa miaka 20 (2026 - 2046) mpango ambao umepitishwa rasmi na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo na mpango huo ukitarajiwa kuanza mapema mwaka huu 2026
Mpango huo wenye lengo la kupanga, kuboresha na kujenga upya eneo la Sinza ili kukidhi mahitaji ya sasa ya kijamii, kiuchumi na kimazingira
Mpango huo utaibadilisha Sinza kutoka kwenye muundo wa majengo mfuto na kwenda kwenye majengo shadidi (Majengo marefu) kupitia dhana ya uunganishaji wa viwanja (block plan)





