"Sio Azam Complex, semeni Muda Complex" - Ali kamwe
Sisti Herman
February 9, 2024
Share :
Mara baada ya baada ya klabu ya Yanga kuondoka na pointi 3 kwa kuifunga mabao 2-1 Mashujaa FC mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Februari 08, 2024 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga SC, Ally Kamwe ameupa jina jipya uwanja wa Azam kwa kuuita “Muda Complex” kwasababu ya mfululizo wa matukio ambayo kiungo wa kati wa timu hiyo Mudathir Yahya anayoendelea kuyafanya kwenye mechi wanazocheza kwenye uwanja huo.
Mabao katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex chamazi yamefungwa na wachezaji Maxi Nzengeli 45', na Mudathir Yahya 86' huku bao la Mashujaa FC likifungwa na Emanuel Mtumbuka 65'.
Mudathir ameutumikia uwanja wa Azam Complex kwa muda mrefu akiwa na Azam Fc kabla ya kuhamia Yanga na ameikomboa Yanga kwenye nyakati ngumu kwenye mechi muhimu kama ile dhidi ya Dodoma jiji msimu uliopita kwa bao la dakika za jioni lililowapa ubingwa, kama hiyo haitoshi wiki iliyopita pia aliipatia Yanga bao la ushindi dakika za mwishoni dhidi ya Dodoma jiji kabla ya mchezo wa jana.