pmbet

Sio mechi, tunaenda kucheza fainali - Zimbwe

Sisti Herman

December 18, 2023
Share :

Nahodha msaidizi wa Simba Mohamed Hussein Zimbwe amesema mchezo wa kesho wa raundi ya 4 ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC wataingia kucheza kama wanacheza fainali na sio mechi ya kawaida kwao.

 

“Mechi tuliyocheza na Wydad kule Marrakech imepita, huu ni mchezo mpya, tunafahamu ugumu wa mechi ya kesho, tunaenda kucheza sio mechi tu ni fainali kwahiyo maandalizi ni mazuri na yale yaliyotokea Morocco waalimu wameona mazuri wameyachukua na mapungufu wameyafanyia marekebisho na naamini tutakua na mechi nzuri na tutaweza kupata matokeo”  alisema Zimbwe kwenye mkutano na wanahabari.

 

Mahojiano haya utayapata kwa urefu zaidi kwenye mtandao wa Youtube wa PMTV.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet