pmbet

SIONDOKI, Biden akataa kujitoa kinyang'anyiro cha Urais wa Marekani

Eric Buyanza

July 4, 2024
Share :

Rais Joe Biden wa Marekani amekataa kujitoa kwenye uchaguzi wa Novemba, wakati kukiwa na shinikizo kumtaka ajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kushindwa kwenye mdahalo wake na Donald Trump wiki iliyopita. Msemaji wake, Karine Jean-Pierre, amekanusha kuwa Biden alimuambia mmoja wa washirika wake wa karibu kwamba uwezekano wa yeye kuchaguliwa tena upo hatarini, endapo atashindwa kurejesha imani ya umma kwake baada ya matokeo mabaya ya mdahalo huo. 

Biden amedai kuwa kushindwa kwake kwenye mdahalo huo kulitokana na kulemewa na majukumu na kuchoka sana katika siku za karibuni. 

Baadhi ya magavana wa chama chake cha Democrat waliokutana hapo jana na Biden, wamesema bado wana imani naye ingawa wamekiri kuwa mdahalo ulikuwa mbaya kwake. 

Rais Biden alikula chakula cha mchana kwa faragha jana na Makamu wa Rais Kamala Harris katika Ikulu ya White House na baadae walijiunga na kampeni huku Biden akiweka wazi kuwa atasalia kwenye kinyang'anyiro hicho. "Mimi ndiye mteule wa Chama cha Democratic. Hakuna mtu wa kuniondoa. Siondoki," alisema, chanzo kiliiambia BBC News. 

Maneno hayo hayo yalirudiwa katika barua pepe ya kuchangisha pesa iliyotumwa saa chache baadaye na kampeni ya Biden-Harris. "Wacha niseme haya kwa uwazi na kwa urahisi niwezavyo: Ninagombea," Bw Biden alisema katika barua pepe hiyo, na kuongeza kuwa atakuwa kwenye kinyang'anyiro hicho hadi mwisho.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet