Sir Kenny Dalglish afichua kufanyiwa matibabu ya Kansa.
Joyce Shedrack
June 2, 2026
Share :
Gwiji wa Liverpool Sir Kenny Dalglish amefichua kuwa anaendelea na matibabu kufuatia kugundulika kuwa na saratani.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 75 alisema alikuwa amepanga kuweka matibabu yake ya faragha lakini bila kukusudia alifichua habari hizo kwenye mitandao ya kijamii.

Katika taarifa yake, Dalglish alisema: "Kama chapisho langu la mtandao wa kijamii lilivyoonyesha bila kukusudia, kwa sasa ninaendelea na matibabu ya saratani.
Liverpool ilitoa taarifa ya kumsapoti, iliyosomeka: “tupo pamoja, kila la kheri, na upendo wa kila mtu katika Liverpool FC, na itaendelea kuwa na Sir Kenny na familia yake.
Dalglish anatajwa sana kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kuichezea Liverpool, akiwa amecheza mechi 515 na kufunga mabao 172 kati ya 1977 na 1990.
Katika kipindi hicho, alishinda mataji matatu ya Kombe la Uropa na mataji manane ya Ligi Daraja la Kwanza huku Liverpool ikitawala soka la Uingereza na Ulaya.





