Sir Ratcliffe anamnyatia beki wa Everton, Jarrad Branthwaite
Eric Buyanza
May 30, 2024
Share :
Manchester United wanamnyatia beki wa Everton mwenye umri wa miaka 21, Jarrad Branthwaite, ambaye thamani yake ni kati ya pauni milioni 60-70 kwa mujibu wa (Sky Sports)
United wanataka angalau beki mmoja mpya wa kati, wakati huu ambao Raphael Varane akijiandaa kuondoka na kuna uwezekano pia wa Jonny Evans kuondoka.
Branthwaite ameibuka kuwa mmoja wa mabeki wazuri chipukizi kwenye Premier League na anaonekana kama aina ya mchezaji anayeweza kubadilisha hali ya United uwanjani.