pmbet

Siri ya uwepo wa uwanja wa Santiago Bernabeu.

Joyce Shedrack

June 2, 2026
Share :

Santiago Bernabéu Yeste siyo jina la uwanja wa Real Madrid tu; huyu ndiye mtu aliyeikuta klabu hiyo ikiwa magofu na kuigeuza kuwa klabu kubwa na yenye mafanikio makubwa zaidi duniani. Maisha yake yalianza tangu mwaka 1909 alipojiunga na timu hiyo akiwa kijana wa miaka 14, akacheza kama mshambuliaji, akawa nahodha, na baadaye akatumikia kama katibu mkuu.
Santiago Bernabéu de Yeste - History and honours | Official website Real  Madrid C.F.

Mwishoni mwa miaka ya 1930, Vita vya Ndani vya Uhispania vilisababisha klabu ya Real Madrid kusambaratika kabisa. Uwanja wao uliharibiwa vibaya na kutumika kama kambi ya kijeshi, mataji yao yalipotea, na klabu ilibaki bila fedha huku mahasimu wao Atletico Madrid wakitawala jiji la Madrid. 

 

Mwaka 1943, Bernabéu alichaguliwa kuwa Rais wa klabu hiyo na kuanza harakati za kuitafuta klabu upya.
Wazo lake la kwanza kubwa lilikuwa kujenga uwanja mkubwa zaidi Ulaya wakati huo ili kupata mapato makubwa. Watu walimcheka na kumwita "mwendawazimu" kwa sababu klabu haikuwa na pesa, lakini alifanikiwa kuuza hisa maalum kwa mashabiki na wanachama kufanikisha ujenzi huo. Uwanja huo ulifunguliwa mwaka 1947, na miaka michache baadaye (1955), bodi ya klabu iliamua kuuita kwa jina lake: Estadio Santiago Bernabéu.
 

Bernabéu aliamini kuwa uwanja mkubwa unahitaji wachezaji wakubwa duniani, hivyo akasajili mastaa wakubwa wa kigeni kama Alfredo Di Stéfano na Ferenc Puskás. Katika kipindi hicho, yeye na waandishi wa habari wa Kifaransa walikaa chini na kubuni mashindano mapya yatakayozikutanisha timu bingwa za Ulaya (European Cup), mashindano ambayo leo yanajulikana kama UEFA Champions League, na Real Madrid ilishinda mataji 5 ya kwanza mfululizo
 

Mzee Santiago Bernabéu alifariki dunia tarehe kama ya leo, Juni 2, 1978, kufuatia ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 82 na akiwa ametumikia klabu hiyo kwa miaka 35 kama Rais . Kifo chake kilitokea wakati fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1978 zikiendelea nchini 

 

Argentina, tukio lililoifanya FIFA kutangaza siku tatu za maombolezo duniani kote na wachezaji wote kuvaa vitambaa vyeusi mikononi kumuenzi.
 

Alipoondoka duniani, aliiachia Real Madrid mataji 16 ya La Liga, mataji 6 ya European Cup (Champions League), na uwanja wa kisasa wenye jina lake. Hakika, yeye ndiye aliyeandika herufi za dhahabu za Real Madrid tunayoiona leo

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet