pmbet

SIRI YAFICHUKA: Jinsi Real Madrid walivyomkosa Messi akiwa na miaka 13

Eric Buyanza

October 31, 2026
Share :

Aliyekuwa Katibu wa Ufundi wa Real Madrid, Miguel Ángel Portugal, amefichua kuwa klabu hiyo ilipata nafasi ya kumsajili Lionel Messi mnamo mwaka 2001, kabla ya mchezaji huyo hatari wa Argentina kuamua kuichezea Barcelona.

 

Miguel ameeleza kuwa Real Madrid walifanya mazungumzo ya siri na baba mzazi wa Messi, Jorge Messi, baada ya kuvutiwa na kipaji kikubwa cha kijana huyo alipokuwa na umri wa miaka 13 tu. Wakati mazungumzo hayo yanafanyika, Messi alikuwa bado hajasaini mkataba wa kudumu na Barcelona, hali iliyotoa mwanya kwa Real Madrid kujaribu kumshawishi ahamie jijini Madrid.

 

Hata hivyo, mpango huo ulikwama kwa sababu Barcelona walikuwa tayari wameahidi kulipia gharama zote za matibabu ya Messi ya kuongeza homoni za ukuaji, jambo ambalo lilikuwa kipaumbele kikubwa kwa familia yake. Mwishowe, Messi alisaini mkataba wake wa kwanza wa kihistoria na Barcelona na kwenda kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya soka duniani.

 

Messi aliongezewa homoni za ukuaji kwa sababu alipokuwa mtoto aligundulika kuwa na ugonjwa wa ukosefu wa homoni za ukuaji mwilini (Growth Hormone Deficiency - GHD).

 

Hali hii ilisababishwa na tezi yake ya pituitari au kitalaam 'pituitary gland' kutozalisha homoni za kutosha za kumuwezesha kukua kawaida kama watoto wengine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet