pmbet

SIRI YAVUJA! Sababu ya Cristiano Ronaldo kufunga ndoa sebuleni

Eric Buyanza

August 17, 2026
Share :

Katika kile ambacho wengi walikuwa hawajui ni kuwa ile ndoa maarufu ya mwanasoka Cristiano Ronaldo na mkewe Georgina Rodríguez ilifungwa kwenye sebule ya nyumba yao, sababu ikielezwa ni kutaka kuacha kumbukumbu ya kipekee kwa watoto wao, pamoja na kutafuta faragha mbali na fujo za vyombo vya habari.

 

Katika mahojiano na jarida la Vogue, Georgina alieleza kuwa walichagua sebule hiyo kwa sababu ndipo mahali wanapoishi maisha yao halisi ya kila siku—mahali wanapokaa pamoja kama familia kupata kifungua kinywa, chakula cha mchana na cha jioni.

 

Kwa mujibu wa Georgina, anataka baada ya miaka 30 watoto wao wakumbuke kuwa kwenye meza hiyo hiyo ya chakula wanayoitumia kila siku, wazazi wao walibadilishana viapo vya ndoa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet