Sisi ndio timu bora zaidi barani ulaya kwa sasa - Marc Cucurella
Eric Buyanza
November 10, 2026
Share :

Beki wa kushoto wa Real Madrid, Marc Cucurella, ametoa kauli nzito akidai kuwa miamba hiyo ya Hispania ndiyo timu bora zaidi barani Ulaya kwa sasa.
Kauli hiyo imeibua mijadala mikubwa kwenye ulimwengu wa soka ikizingatiwa kuwa timu yake haijakaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Hispania (La Liga) wala kundi lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Cucurella alitoa msimamo huo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha redio cha El Partidazo kinachorushwa na kituo cha Cope cha nchini Hispania.
"Kwa mtazamo wangu, sisi ndio timu BORA zaidi barani Ulaya kwa sasa. Tumekuwa na mfululizo mzuri sana wa matokeo na timu imeanza kucheza kwa nidhamu na umakini mkubwa sana," alisema Cucurella wakati akizungumza na Cope.
Alipoulizwa kama Real Madrid ni bora kuliko matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG), Cucurella alijibu kwa kifupi: "Wana timu nzuri sana, lakini ukweli ni kwamba siangalii mechi zao. Kwangu mimi, timu bora zaidi Ulaya kwa sasa ni Real Madrid."





