"Sisi so milima tutakutana..." Hatimaye wamekutana
Sisti Herman
January 11, 2024
Share :
Baada ya wiki 2 klabu ya Inter Miami ya ligi kuu soka nchini Marekani kukailisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Luis Suarez ni rasmi sasa anakutana na marafiki zake waliokuwa wote Catalunya, Lionel Messi, Sergio Busquet na Jordi Alba.
Kama hiyo haitoshi pia Inter Miami wamechapisha kupitia mitandao yao ya kijamii picha ya pamoja ya watoto wa mastaa hao ambao walikuwa marafiki zamani huku wakiwa wamevalia jezi zenye majina ya wazazi wao yaani Aba, Messi, Sergio na Suarez.
Ama kweli “Sisi sio milima, tutakutana tu” nani angedhani kuwa mastaa wangeweza kukutana mwishoni mwa maisha yao ya soka la ushindani.