Sisi tupo tayari kula hiyo nyama ya Tembo – Mbunge
Eric Buyanza
June 3, 2024
Share :
Katika hali ya kushangaza Mbunge wa Viti Maalum, Dk Thea Ntara, amesema kama serikali inafikiria kupunguza wanyama wakorofi wakiwemo tembo wanaovamia makazi ya watu ni vyema wakawaua, kisha nyama yake wakapewa wananchi kama mboga.
”Lakini pia Mheshimiwa Waziri, suala la tembo, Ruvuma tunakula sana nyama ya tembo. Hebu niwaombe kama mnafikiria kupunguza, muwachinje sijui niseme kuwaua, halafu tengenezeni hizo nyama, pelekeni mikoa ambayo tembo wanaliwa.
“…Mjipange kuhusu hawa wanyama wanaoua wapunguzeni, sisi tupo tayari kula hiyo nyama,” amesema Mbunge huyo.