pmbet

Sita mbaroni wakihusishwa na mauaji ya Rapa 'AKA'

Eric Buyanza

February 28, 2024
Share :

Washukiwa sita wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Afrika ya Kusini wakisubiri kufikishwa mahakamani kufuatia mauaji ya rapa Kiernan Forbes, maarufu AKA.
 

Akitoa taarifa hiyo Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa KwaZulu-Natal, Lt Jenerali Nhlanhla Mkhwanazi alieleza kuwa watu hao walilipwa kufuatilia kila hatua za rapa huyo kabla ya kumtoa nje ya mgahawa pamoja na rafiki yake ambaye alikumbwa kwa bahati mbaya katika sakata hilo la mauaji.
 

"Ilikuwa wazi kwamba AKA alifuatiliwa kutoka uwanja wa ndege, na Tibz hakuwa mlengwa aliyekusudiwa katika mauaji kwenye Barabara ya Florida huko Durban. Tunajua walilipwa kwa hili,” Lt Jenerali Mkwananzi alisema.
 

AKA alipigwa risasi na mtu asiyejulikana dakika chache baada ya kutoka nje ya mgahawa aliokuwa akila huko jijini Durban.

Kifo cha rapa huyo kilitikisa Afrika na dunia nzima haswa kwa wale wafuatailiaji wa muziki wa Hihhop.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet