pmbet

Sitaki kusikia kesi za mimba walimu tutakabana shingo.

Joyce Shedrack

September 27, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma kulinda maadili ya watoto na kusisistiza kuwa hataki kusikia kesi za mimba kwa wanafunzi.

"Hakikisheni mnalinda maadili ya watoto wetu sitaki kusikia kesi za mimba shuleni hapa, huku msituni mimba itatokea wapi? Ukitokea ujauzito, walimu tutakabana shingo kwa sababu huku msituni hakuna pa kutokea mimba," ameongeza kwa msisitizo.

Rais Samia amezungumza hayo mara baada ya kuzindua shule hiyo leo tarehe 27 Septemba, 2024 akisisitiza kuwa walimu wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafunzi wanajifunza vizuri na wanatunzwa kiakili, kiafya, na kijamii.

"Walimu, tumewakabidhi watoto wetu. Mazingira ya shule ni mazuri, shule yenyewe ni nzuri, na ingawa tutahitaji kuongeza idadi ya walimu kadiri wanafunzi wanavyoongezeka, bado ninaomba sana kuwa walimu muwatunze watoto hawa. Mungu amewachagua kuwa walezi wa hawa watoto, hakikisheni mnawajenga kielimu, kiafya, na kuwawezesha kujitambua kama wanawake wenye uwezo wa kufikia ndoto zao," amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia aliwahakikishia walimu kuwa serikali inatambua changamoto wanazokutana nazo, ikiwemo uhaba wa maslahi, na akawataka kuwa na subira huku serikali ikiendelea kuzifanyia kazi.

"Tunajua changamoto zenu, tunajua masilahi yenu yapo chini, lakini tunaendelea kuzifanyia kazi ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanaimarika," amesema Rais Samia.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet