Sitaki 'kuweka ratiba’ vita vya Iran vitaisha lini – Netanyahu
Eric Buyanza
March 31, 2026
Share :

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa zaidi ya nusu ya malengo ya kijeshi dhidi ya Iran tayari yamefikiwa, lakini hakutaka “kuweka muda maalum” wa lini vita hivyo vitamalizika.
Netanyahu anasema vita "bila shaka nusu ya vita imepita" na jamhuri ya Kiislamu ya Iran hatimaye "itaanguka," shirika la habari la AFP linaripoti.
Kiongozi huyo wa Israel pia amesema kuwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanaendelea kudhoofisha uongozi wa Iran.
Wakati huo huo Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa limetambua makombora yaliyorushwa kutoka Iran kuelekea Israel, na kwamba mifumo ya ulinzi wa anga kwa sasa inafanya kazi "kuzuia tishio".
Tahadhari imetolewa kwa umma, kuwasahauri watu kuelekea maeneo salama ya " kujikinga dhidi ya makombora" na kusalia hapo hadi ilani nyingine itakapotolewa.
BBC





