pmbet

Sitashagaa Mzize akibeba kiatu cha dhahabu - Miloud

Eric Buyanza

April 23, 2025
Share :

Huku timu yake ikiendelea kujiimarisha katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi, amemwagia sifa, Clement Mzize na kusema anatarajia mshambuliaji huyo atafunga mabao mengi zaidi na kutwaa tuzo ya mfungaji bora msimu huu.

 

Mzize alifunga mabao mawili na kufikisha idadi ya magoli 13 wakati Yanga SC ikipata ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, Mkoani Manyara.

 

Miloud alisema Mzize yuko katika kiwango cha juu hivi sasa na wala hatashangaa kuona akitwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu msimu huu.

“Nimefurahishwa na kiwango cha Jonathan Ikangalombo, ambaye aliingia na kutoa asisti, Stephane Aziz Ki, amefunga na kutoa ,asisti’ pia, pongezi kwa Dube (Prince), lakini asante sana kwa Mzize, amekuwa kwenye kiwango kikubwa na cha hali ya juu kwa sasa, natarajia atafunga mabao mengine mengi zaidi na kuibuka kuwa mfungaji bora msimu huu,” alisema kocha huyo.
 

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet