Sitauacha muziki wa Taarab hadi naenda kaburini – Mzee Yusuph
Eric Buyanza
July 25, 2024
Share :
Akijibu swali ikiwa yuko tayari kuacha tena muziki kama alivyofanya siku za nyuma? Mkongwe kunako muziki wa Taarab Mzee Yusuph alisema hiviii;
“Katika vitu ambavyo siwezi kukosea tena, ni kuuacha huu muziki wa taarabu, sitauacha hadi naenda kaburini, sitaki kuwakosea tena mashabiki zangu na wao wameshaniambia nikiwaacha tena nikirudi hawatanipokea, hivyo niko nao sambamba jino kwa jino ama kuzikwa na kuzikana.”
MWANASPOTI