"Situmii watunzi wa nyimbo" - Burna Boy amjibu msanii wa Davido
Eric Buyanza
July 8, 2024
Share :
Mwanamuziki kutoka Nigeria na mshidi wa tuzo za Grammy, Burna Boy, amekana kutumia watunzi wa nyimbo kwenye kazi zake kama ilivyoripotiwa na msanii Logos Olori kutoka lebo ya Davido (DMW).
Akiongea karibuni kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Radio nchini humo, Logos alisema wasanii wakubwa wa Nigeria kama Burna Boy na Wizkid pia hutumia watunzi kwa ajili ya kuwaandikia nyimbo zao.
Hayo yamejiri siku chache baada ya bosi wake, Davido kuandamwa kwenye mitandao ya kijamii ya kwamba eti anajidai mwanamuziki mkubwa wakati anatumia watunzi kumuandikia nyimbo.
Kwenye mahojiano hayo Logos alisema hivi kwa wale wanaomshangaa bosi wake kutumia watunzi;
“Wengi wanaoshangaa wasanii kutumia watunzi wa nyimbo hawajui mengi kuhusu biashara ya muziki. Mwanamuziki mara nyingi anaandika nyimbo zake siku zake za mwanzo wakati ndio anatoka kimuziki.
Unapokuwa na maonyesho 10 kwa wiki katika nchi tofauti, ndio utaelewa kuwa unahitaji mtunzi” alisema Logos.