Siuchukulii muziki kama kazi, nauona kama mtindo wa maisha
Eric Buyanza
July 14, 2025
Share :
Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Burna Boy, amesema kwa upande wake hauchukulii muziki kama kazi.
Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC Radio 1 Xtra, msanii huyo alisema anapenda kuwa mwanamuziki na anauchukulia kama mtindo wa maisha badala ya kazi, na kutokana na hilo haoni sababu yoyote ya kwenda likizo kwa kuwa muziki ni mtindo wa maisha kuliko taaluma kwake.
"Naipenda kazi yangu. Siichukulii kazi yangu kama kazi. Ninaiona kuwa maisha. Kwa nini nihitaji likizo kwenye maisha? anahoji msanii huyo.