'Sivutiwi tena na mauzo wala Chati za Muziki' - Beyonce
Eric Buyanza
June 22, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa Marekani, Beyonce ameibuka na kusema siku hizi hahamasishwi tena na chati za muziki wala mafanikio ya mauzo ya kazi hizo.
“Kuna wakati maishani mwangu chati na mauzo yalinisisimua na kunitia moyo” alisema Beyoncé alipokuwa kwenye mahojiano na The Hollywood Reporter.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 42 aliyejaaliwa watoto 3 na mume wake rapa maarufu Jay Z, anasema hata hivyo ukuaji wake kwenye tasnia hiyo ndio uliobadilisha mtazamo wake juu ya mafanikio katika muziki.
Beyonce ambaye aliingiza sokoni albam yake mpya ‘Cowboy Carter' March 29, 2024
anasema anashukuru kwa mafanikio ya kushangaza ya albamu hiyo ambayo imebadilisha maisha yake.