pmbet

"Siwezi kuoa mwanamke ambaye si bikira" - Seneta Ned Nwoko

Eric Buyanza

March 19, 2024
Share :

Mume wa muigizaji maarufu wa filamu za kinigeria (Regina Daniels), Bilionea Ned Nwoko, amefichua siri yake kubwa kuwa alioa wake zake wote sita akiwemo Regina wakiwa mabikira. 

Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Bilionea huyo amesema alishajiwekea nadhiri kuwa katika maisha yake hataoa mwanamke ambaye sio bikira. 

“Nilipokutana na Regina sikufahamu yeye ni nani kwa sababu huwa siangalii sinema za Uingereza, Nigeria au Marekani, pia mimi si mtu wa mitandao ya kijamii, hadi wakati huo sikuwa na Akaunti za Facebook au Instagram. 

"Kwa hiyo, sikujua kuhusu Regina hadi alipokuja nyumbani kwangu na familia yake, nilimpenda nilipomwona kwa mara ya kwanza na haswa nilipogundua kuwa anatoka kijijini kwetu kwasababu siku zote nilitaka kuwa na mke kutoka upande wangu"

Bilionea huyo anasema alipogundua kuwa Regina ni bikira, ilimhamasisha sana kutaka kumuoa kwasababau alioa wake zake wote wakiwa mabikira.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet