"Siyo Messi wala Ronaldo, mchezaji bora wa muda wote ni Zidane" - Hazard
Sisti Herman
February 20, 2024
Share :
Akiwa kwenye mahojiano na Podcast maarufu ya kiungo wa kati wa zamani wa Nigeria na Chelsea Mikel Obi, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na timu ya Taifa ya Ubelgiji Eden Hazard amekiri kuwa nyota wa zamani wa Ufaransa na Real Madrid Zenedine Zidane ndiye mchezaji wake bora wa muda wote.
Hazard amesema hayo alipoulizwa kuwa kati ya Ronaldo na Messi nani ni mchezaji wake bora wa muda wote, akajibu “kwa upande wangu mchezaji bora wa muda wote sio kati ya hao uliowataja, kwangu ni Zidane” alimaliza Hazard ambaye amestaafu rasmi kuchezea soka baada ya majeraha ya mara kwa mara.