Skendo za TB Joshua zaibuka
Sisti Herman
January 9, 2024
Share :
Kwa mujibu wa uchunguzi ulioripotiwa na BBC, umedaiwa kuwa kiongozi la wa kanisa la Sinagogi la Mataifa Yote (SCOAN) marehemu TB Joshua aliwanyanyasa kingono na kimwili baadhi ya waumini wake ikiwemo Kuwapiga na Kuwafunga na Minyororo.
Zaidi ya watumishi na waumini 25 wa kiongozi huyo waliohojiwa na BBC kutoka Mataifa ya Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani wamedai walianza kufanyiwa vitendo hivyo wakiwa na umri kati ya miaka 17 na 25 na wengine kulazimika kutoa ujauzito zaidi ya mara 5.
Kabla ya Kifo chake mwaka 2021, Marehemu TB Joshua alikuwa akitajwa miongoni mwa Wahubiri wenye ushawishi mkubwa Duniani huku akijizolea wafuasi wengi kupitia Vipindi vya Runinga vya Emmanuel TV.