Skudu atangaza kustaafu soka ageukia ukocha.
Joyce Shedrack
July 16, 2026
Share :
Winga wa Afrika Kusini, Mahlatsi Skudu Makudubela ametangaza rasmi kustaafu soka la ushindani baada ya kuwa na safari ya mafanikio iliyodumu kwa miaka 17 huku akiweka wazi safari ya ukocha inafuata.

Katika kipindi chote cha maisha yake ya soka, Makudubela aliwahi kuzitumikia klabu mbalimbali zikiwemo Platinum Stars, Mamelodi Sundowns, Marumo Gallants pamoja na klabu ya Yanga.
Skudu alijizolea sifa kutokana na kasi yake, uwezo mkubwa wa kupiga chenga na ubunifu uliowapa wakati mgumu mabeki wa wapinzani huku akifanikiwa pia kutwaa mataji mbalimbali, likiwemo Kombe la MTN8 akiwa na Platinum Stars pamoja na ubingwa wa NBC Premier League Tanzania akiwa na Yanga.
“Baada ya miaka 17 ya kucheza soka la ushindani siku ya leo ninatangaza rasmi kustaafu soka”Ameandika Skudu kupitia ukurasa wake wa Instagram.





