Slemani Mwalimu kuikosa mechi ya dhidi ya Simba leo.
Joyce Shedrack
August 12, 2026
Share :
Nyota mpya wa Yanga Selemani Mwalimu, hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachokutana na Simba leo kwenye Ngao ya Jamii.

Klabu ya Yanga tayari imekamilisha usajili wa Selemani Mwalimu na kupata vibali vinavyohitajika kutoka Wydad Casablanca. Hata hivyo, mshambuliaji huyo hajawa kwenye mpango wa kocha kwa mchezo wa leo.
Selemani amefanya mazoezi rasmi mara moja tu akiwa na Yanga, hivyo bado hajaiva kwa asilimia 100 kushiriki mchezo huo.Kwa taarifa hizo, Selemani anatarajiwa kuanza kuitumikia Yanga katika mechi za Ligi Kuu ya NBC.





