pmbet

Snoop Dogg kushiriki mbio za mwenge.

Joyce Shedrack

July 24, 2024
Share :

Rapa maarufu wa Marekani Snoop Dogg atakuwa miongoni mwa wasanii wachache watakoubeba Mwenge wa Olimpiki katika hatua za mwisho za safari ya mwenge huo kabla haujapelekwa kwenye kivutio maarufu cha Eiffel Tower kilichopo jijini Paris, Ufaransa ikiwa ni shamra shamra za ufunguzi wa mashindano ya olimpiki.

Snoop amewasili jijini Paris kama mwandishi maalumu wa michezo kutoka shirika la NBC ambalo ni mshirika wa Shirika la habari la Sky.



Kupitia mtandao wa X, Snoop (52) alichapisha picha yake akiwa nje ya hoteli iliyoambatana na maneno ” Mko tayari? Paris 2024 Olympics...”.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari Nchini humo vinasema rapa huyo ataubeba mwenge huo kupitia kitongoji cha Saint-Denis ambapo kutafanyika tamasha ikiwa ni kituo cha mwisho kabla ya mwenge huo kuelekea Eiffel Tower.

Mwenge huo uliwashwa mwezi Aprili nchini Ugiriki, katika eneo ambalo ndipo ilipozaliwa michezo ya Olimpiki.
 

Wasanii wengine ambao watashiriki kuubeba mwenge huo siku ya ijumaa kwenye ufunguzi wa mashindano hayo makubwa ni pamoja na rapa MC Solaar, Muigizaji Laeticia Casta,  muongozaji wa filamu Alice Diop, Paralympian Charles-Antoine Kouakou na mchezaji wa mchezo wa rugby Abdelatif Benazzi.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet