Soja wa Nigeria apigwa K.O, Mwakinyo atuma salamu kwa Kiduku
Sisti Herman
January 28, 2024
Share :
Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo usiku wa jana amefanikiwa kushinda mkanda wa WBO Africa Middle Weight baada ya kumtwanga kwa K.O ya raundi ya 7 bondia kutoka Ghana, Elvish Ahorgah kwenye pambano la Mtata Mtatuzi lililopigwa ndani ya Indoor ya New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.
Mwakinyo amesema “Elvis sio Bondia rahisi na hajawahi kupoteza kwa KO hii ni ya mara yake ya kwanza na ni Bondia ambaye anacheza kilo 78 Mimi nimempandia uzito ni kiu changu cha muda mrefu lakini nilitaka kuwaprove WBO kwamba mwili wangu na uwezo nilionao ni vitu tofauti”
“Lakini pia nilikuwa nataka kutuma salamu Morogoro kwa Watu ambao walikuwa wanaamini naogopa zile piko kama Mabibi harusi wa huku , nilikuwa nataka kutumia hii fursa kama mfano wa kuonesha kwamba dau likifikwa ambalo lipo katika makubaliano yangu Mimi na Timu yangu pambano litapigwa hata la kirafiki ili tuone nani ni nani!?” alimaliza hivyo Mwakinyo kupitia shirika la utangazaji Zanzibar, ZBC.