Solanke Mchezaji bora wa mwezi EPL
Sisti Herman
January 12, 2024
Share :
Kocha mkuu wa Aston Villa, Unai Emiry amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi wa ligi kuu Uingereza kwa mwezi wa 12 huku mshambuliaji wa FC Bournemounth Dominic Solanke akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi huo.
Unai Emery amesaidia Villa kushinda mechi 4 kati ya 7 alizowaongoza kwa mwezi huo huku Solanke akifunga mabao 6 na kuisaidia Bournemouth kushinda mechi 4 kati ya 7 za mwezi huo.