pmbet

Solskjaer awatikisa mashabiki Man U: "Kama familia ikiniita, nitarudi"

Eric Buyanza

November 2, 2026
Share :

Aliyekuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Norway na kocha wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amekiri kuwa yuko tayari na ana shauku kubwa ya kurejea klabuni hapo kama meneja iwapo atahitajika tena.

 

Solskjaer, ambaye alidumu klabuni hapo kwa miaka mitatu kama kocha kabla ya kuondoka Novemba 2021, ameweka wazi hisia zake akisema, "Kama familia ikikuomba, unasema ndio." Kauli hii imezua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa mashetani hao wekundu.

 

Mnorway huyo mwenye umri wa miaka 51 bado anapendwa sana na mashabiki wa United kutokana na historia yake kubwa kama mchezaji, hususan goli lake la ushindi katika fainali ya UEFA Champions League ya mwaka 1999, na mtazamo wake chanya aliouleta klabuni hapo alipokuwa kocha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet